Dar es Salaam Tanzania. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe jana September 28,2017 alitembelea uwanja wa taifa kufanya ukaguzi wa kiwanja mabacho kilikuwa kinafanyiwa matengenezo na kampuni ya michezo ya kubashiri nchini ijulikana kama SportPesa Limited.
Akizungumza na waandishi wahabari Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe alisema, `
“Sisi kama serikali na wizara tupo tayari kufanya kazi na kampuni yoyote ambayo inakuja nchini hapa na dhamira njema ya kufanya biashara na moja ya kampuni tuliyoshirikiana nayo ni SportPesa, kwa sababu hata wao wakati wamekuja mwanzoni walieleza kuhusu aina ya mchezo wanayofanya na sisi kama wizara tukawaambia tunatatizo hapa kiwanja inabidi kitengenezwe, tukaweka makubaliano ili kufanikisha hili, Kiukweli kampuni ya SportPesa inajitahidi sana kuendeleza michezo nchini”
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa SportPesa Tanzania Ndugu Tarimba Abbas alianza kwa kuishukuru serikali kwa kuwa bega kwa bega tangu kuanzishwa kwa kampuni mpaka sasa.
“Ushirikiano wetu na serikali ndio umefanya tuweze kutimiza ndoto yetu kubwa ambayo ni kuona Tanzania inapiga hatua kwenye sekta ya michezo na ndio maana tunaendelea kuwaomba mtuunge mkono ili kwa pamoja tuweze kusaidiana kutimiza ndoto hii”
“Marekebisho ya uwanja bado yanaendelea na tunatarajia kukamilika na kukabidhi mwezi Novemba mwaka huu, gharama zitakazotumika mpaka kukamilika kwa ukarabati huu ni shilingi Bilioni 1.3 TZS, hii ni mjumuisho wa ukarabati wa uwanja, vifaa, mishahara ya wataalamu na vitendea kazi kwa muda wa mwaka mmoja.”
MAGOLI YOTE: Mbao FC vs Simba FC September 21 Mwanza (2-2)