Usiku wa September 28 2017 michuano ya UEFA Europa League hatua ya makundi iliendelea tena barani Ulaya, mchezo kati ya BATE Borisov dhidi ya Arsenal ni miongoni mwa michezo ya UEFA Europa League iliyochezwa usiku huo wa September 28.
Arsenal walikuwa ugenini katika uwanja wa Borisov Arena kucheza dhidi ya wenyeji wao BATE Borisov, pamoja na Arsenal kuwa ugenini na BATE Borisove kuizidi Arsenal kwa sapoti kubwa ya mashabiki wao lakini Arsenal walifanikiwa kupata ushindi wa magoli 4-2.
Pamoja na ushindi huo lakini Arsenal walifanikiwa kuutawala mchezo kwa asilimia 62 na BATE Borisov kuutawala mchezo kwa asilimia 38, magoli ya Arsenal yalifungwa na Theo Walcott dakika ya 9 na dakika ya 22, Robert Holding dakika ya 26 na Oliver Giroud dakika ya 49.
Magoli ya BATE Borisov yalifungwa na Mirko Ivanic dakika ya 28 na Mikhail Gordeychuk dakika ya 67, ushindi huo sasa unaifanya Arsenal kufikisha jumla ya point sita na kuongoza kundi lao wakifuatiwa na Crven Zvezda wenye point nne.
Matokeo ya game zote za UEFA Europa League zilizochezwa usiku wa September 28 2017 barani Ulaya #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/pYpWlQJW41
— AyoTV (@AyoTV) September 28, 2017
MAGOLI YOTE: Mbao FC vs Simba FC September 21 Mwanza (2-2)