Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Jakaya Kikwete ya Magonjwa ya Moyo JKCI Prof Mohammed Janabi ameeleza kuwa mtu anapopata mshtuko wa moyo, mshipa huo usipozibuliwa ndani ya dakika 90 mtu huyo lazima atapoteza maisha.
Amesema hayo wakati Shirika la POSTA likitoa msaada wa pesa ya matibabu watoto wawili wenye ugonjwa wa moyo katika taasisi hiyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya POSTA duniani.
“Mpime afya zenu kwani hata kama una pesa nyingi, na ukakosa huduma ya haraka ya kuzibuliwa mshipa huo na madaktari lazima utapoteza uhai hivyo ni vyema watu kupima mara kwa mara kujua hali ya afya zao” – Prof Janabi
Ulipitwa na hii? “Asilimia 12 ya vifo vyote nchini hutokana na saratani ya matiti” – Wizara ya Afya