Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele amekaa na AyoTV na kuzungumzia umuhimu wa baadhi ya makundi ya watu kupimwa matumizi ya dawa za kulevya.
Makundi aliyoyataja Mkemia Mkuu wa Serikali ni pamoja na wafanyakazi wanaoendesha mitambo na magari, wanafunzi wanaoenda kwenye vyuo vikuu kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu.
‘Mwajiri yeyote kabla hujakabidhi vifaa nyeti kwa wafanyakazi wako ni vizuri ukawakagua matumizi ya dawa za kulevya ili kuhakikisha akili zao ziko timamu, wanafunzi wanaokwenda kwenye vyuo vikuu ni vizuri wakapima matumizi ya dawa za kulevya ili Serikali isipoteze rasilimali kuwapeleka kwenye masomo’-Mkemia Mkuu wa Serikali
Unaweza kubonyeza playa hapa chini kuitazama video hii hapa chini
MFUMUKO WA BEI: Ofisi ya Taifa ya takwimu yatoa taarifa ya mwezi September 2017, Bonyeza play hapa chini kutazama