Maelfu ya wanafunzi Italy wafanya mgomo wa kushinikiza serikali kuondoa mfumo wa mafunzo kwa vitendo yaani ‘field’ wakati wa masomo kwa kusema kuwa mafunzo hayo hayana msaada wowote kwa kazi wanazotaka kuzifanya kwa siku za usoni.
Mtandao wa Wanafunzi nchini humo umeeleza kuwa wanafunzi wamechoshwa kufanya kazi pasipo malipo yoyote ambapo wamesema asilimia 95 ya shule zote takriban wanafunzi 900,000 wanafanya kazi za aina hiyo wakati nchi yao ikiendelea kuwa ya 3 katika nchi za Umoja wa Ulaya ambazo zina idadi kubwa wa watu wasio na ajira.
Wanafunzi hao wameitaka serikali ikumbuke ahadi yake ya kutengeneza sheria ambayo itaweka wazi hatma ya watu wanaofanya kazi kwa muda kwenye makampuni mbalimbali kwa ajili ya uzoefu huku ikiwataka wamiliki wa makampuni hao kuwajibika kuwalipa watu hao.
Ulipitwa na hii? Rais JPM: “Kama Aga Khan imesamehewa kodi, mbona gharama za huduma bado ziko juu?”