Unaambiwa nguzo za umeme zimedondoka maeneo ya Mwembeyanga barabara ya Tandika-Posta ambapo kondakta wa daladala iliyohusika kwenye tukio amesema walikua wakisikia vitu kama cheche vinatoka kwenye nguzo hizo.
Baada ya kusikia wakashuhudia nguzo ya kwanza ikidondoka ikifatiwa na ya pili mpaka ya tatu na katika hali ya kujihami, dereva wa gari hiyo aliamua kuingiza gari kwenye mtaro kuukwepa umeme huo uliokuwa bado upo kwenye nyaya hizo zilizolala chini.