Wafuasi 12 wa Chadema wameachiwa kwa dhamana baada ya kusomewa mashtaka mawili ikiwemo ya kufanya fujo katika Mahakama ya Mwanzo Maromboso Arusha.
Wafuasi hao wameachiwa mbele ya Hakimu Obadia Mongi baada ya upande wa mashtaka kuwasomea makosa yao washtakiwa.
Washtakiwa wanakabiliwa na makosa mawili, kufanya fujo katika kampeni za udiwani na kufanya shambulio la kawaida.
Baada ya kusomewa makosa hayo, washtakiwa walikana ambapo mahakama iliwapatia masharti ya dhamana ya kuwa na barua za utambulisho kutoka kwa Mtendaji wa Kata na nakala ya kitambulisho cha mpiga kura.
Pia wametakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Tsh.600,000 kila mmoja, ambapo walifanikiwa kutimiza masharti hayo na kuachiwa kwa dhamana. Kesi imeahirishwa hadi November 16,2017.
Ulipitwa na hii? Baada ya mwaka na nusu, upelelezi kesi ya Kitilya bado