Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo November 9, 2017 alisimama Bungeni Dodoma kujibu maswali ya papo kwa papo, Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea alisimama kutaka kujua swala la katiba mpya limefikia wapi?
Mtolea alihoji kwa kusema “Katika Serikali ya awamu ya nne Nchi hii ilitumia Mabilioni ya fedha kuzunguka nchi nzima kukusanya maoni ili kuandaa Katiba mpya, hii ilikuja baada ya kugundua taifa linahitaji Katiba mpya kutibu changamoto nyingi ikiwemo kulinda rasilimali, haki za Binaadamu n.k”
“Tunaipongeza Serikali ya awamu ya nne kwa kuanzisha mchakato ule pamoja na changamoto zilizojitokeza baadae, sasa Serikali ya awamu ya tano toka imeingia madarakani leo ni miaka miwili imepita haijafanya jambo lolote la kuendeleza mchakato ule, Mh. Waziri Mkuu naomba waambie Watanzania leo nini mpango wa Serikali ya awamu ya tano katika kutimiza ndoto za Watanzania kupata katiba mpya”
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim alimjibu kama ifuatavyo….. “Swala la katiba mpya linahitaji gharama kubwa ya fedha na zinatokana na mapato yanayokusanywa ndani ya nchi lakini kila mwaka wa fedha una vipaumbele vyake na sisi tumejikita katika kutoa huduma za jamii kwa Wananchi“
“Tumekua tukishuhudia Watanzania wanahitaji maji vijijini, afya, elimu, miundombinu ili kuwawezesha Watanzania kuendelea na maisha yao, Katiba ni muongozo unaelekeza mambo kadhaa… sasa hivi tunayo katiba ambayo ina miongozo ileile ingawa tumekusudia kuibadilisha”
Kufahamu kila kitu alichosema Waziri Mkuu Majaliwa bonyeza play umtazame kwenye hii video hapa chini…
MBOWE VS MAJALIWA BUNGENI: Kuhusu kushambuliwa kwa Tundu Lissu na wengine, bonyeza play hapa chini kutazama
UNAZITAKA BREAKING NEWS FASTAFASTA? Jiunge na Reporter wako Millard Ayo kwa kubonyeza kifuatacho SUBSCRIBE >>> YOUTUBE , APP YA MILLARD AYO, FACEBOOK , INSTAGRAM