Wataalamu wa afya nchini Japan katika uchunguzi wao walioufanya kwa miaka kadhaa wameeleza kuwa tabia ya kula chakula harakaharaka humfanya mtu anayekula hivyo kuwa kwenye hatari ya magonjwa ya uzito uliopitiliza, shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.
Utafiti huu umegundua kuwa wale wanaokula harakaharaka huwa kwenye hatari ya magonjwa hayo mara tano zaidi ya wanaokula polepole.
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo Takayuki Yamaji ambaye pia ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Hiroshima nchini Japan ameeleza kuwa ulaji wa haraka hupelekea kuongezeka uzito, glukosi nakuongeza upana wa kiuno.
Utafiti tofauti na huo uliofanywa miaka michache iliyopita na North Carolina State University ulionyesha kuwa watu wanaokula chakula huku wametulia na ku-enjoy utamu na harufu yake huweza kupungua uzito kwa haraka na hivyo kushauri watu kuwa na tabia ya kula chakula bila kujihusisha na shughuli zozote kama kutazama TV au wakiwa wana kazi nyingine.
ULIPITWA? ALICHOANDIKA PAUL MAKONDA BAADA YA LULU KUHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA