Mechi kati Simba na Rhino Rangers imemalizika kwa ushindi wa goli 1 la Simba dhidi ya 0 kwa Rhino Rangers kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mechi iliyomalizika jioni hii Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa Ushindi huu unaifanya timu ya Simba SC itimize pointi 28 baada ya kucheza mechi 14 ikibaki nafasi ya 4 nyuma ya Yanga ambayo yenye pointi 31 Azam na Mbeya City pointi 30 kila moja.
Hadi mapumziko tayari Simba SC walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0 lililofungwa na mshambuliaji Ramadhani Yahya Singano ‘Messi’ dakika ya 14
Pamoja na kufungwa Rhino walionekana kucheza vizuri na kuonyesha upinzani kwa Simba ambao katika mechi ya mzunguko wa kwanza walitoka nayo sare ya 2-2 mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyhi Tabora.
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa na wachezaji wafuatao; Ivo Mapunda, Haruna Shamte, Idrisa Rashid, Gilbert Kaze, Donald Mosoti, Awadh Juma, Haruna Chanongo, Amri Kiemba, Ali Badru/Said Ndemla dk, Amisi Tambwe/Betram Mombeki aliyeingia dk65/Henry Joseph aliyeingia dk85 na Ramadhani Singano ‘Messi’.
Kwa upande wa Rhino Rangers wachezaji wake walikua ni; Charles Mpinuki, Julius Masunga, Amani Juma, Ladislaus Mbogo, Laban Kambole, Hamisi Msafiri, Salum Kamana, Hussein Abdallah, Darlingtn Enyinna, Suleiman Jingo/Salum Majid dk84 na Shijja Mongo.