Jumamosi ya December 9 2017 timu ya taifa ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars ilihitimisha safari yake ya kuwania Kombe la CECAFA nchini Kenya kwa kucheza mchezo wake wa tatu wa Kundi lao dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda.
Kwa bahati mbaya Tanzania bara wamepoteza mchezo wao wa pili leo kwa kuruhusu kufungwa na Rwanda magoli 2-1, magoli ya Rwanda yalifungwa na Innocent Nshuti dakika ya 17 baadae Daniel Lyanga akasawazisha dakika ya 29 ila Biramahire Abedy dakika ya 66 akazima ndoto za Tanzania kwa kuifungia Rwanda goli la pili.
Kilimanjaro Stars inaondolewa katika michuano ya CECAFA ikiwa na point moja iliyoipata katika sare tasa 0-0 dhidi ya Libya lakini game zake mbili ameambulia kipigo ikiwemo ya Zanzibar Heroes aliyofungwa goli 2-1, baada ya kutolewa kocha wa Kilimanjaro Stars Ammy Ninje aliongea hivi.
“Najivunia tulicheza mchezo mzuri lakini mwisho wa siku tulipoteza mchezo tutajifunza katika mashindano kama haya kuwa ni lazima upate matokeo nawaambia nini watanzania? Always Next Time”>>> Ammy Ninje
Kocha wa timu ya Tanzania Bara Kilimanjaro Stars Ammy Ninje baada ya kutolewa katika michuano ya CECAFA kwa kufungwa 2-1 dhidi ya Rwanda #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/3V6XLLOxLS
— AyoTV (@AyoTV) December 9, 2017
VIDEO: Atayofanya Mo Dewji kwa Simba ndani ya mwaka mmoja