Leo December 15, 2017 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, kimetangaza majina ya watakaogombea katika uchaguzi wa Ubunge katika Majimbo matatu ambayo ni Singida Kaskazini, Songea Mjini na Longido.
“Kamati Kuu baada ya uchambuzi na tathmini ya kina kwa walioomba dhamana na kwa kuzingatia misingi ya maadili, uchapakazi, uwakilishi bora kwa wananchi, imewateua, Monko Justine Joseph kugombea Singida Kaskazini,” – POLEPLE
“Damas Daniel Ndumbaro kugombea Songea Mjini na Dkt. Stephen Lemomo Kiruswa kugombea jimbo la Longido, chama kinawatakia maandalizi mema ya uchaguzi,” -POLEPOLE
EXCLUSIVE: KAULI YA LOWASA KUHUSU BABU SEYA KUACHIWA, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA