Ni headline kutokea mkoani Geita ambapo Mkuu wa mkoa huo Robert Gabriel ametangaza kuzuia likizo kwa watumishi wake wote hadi utakapokamilika mpango wa ujenzi wa madarasa ya wanafunzi wa sekondari.
Akiongea na Ayo TV katika Exclusive interview RC Robert amesema…>>>”Ni kweli nimezuia likizo zote kwa watumishi wangu, sasa kama wewe ni Afisa elimu, Mwalimu Mkuu, Mkurugenzi unaenda likizo mwezi January na hujapokea wanafunzi wala hujui watakaa wapi your not serious”
“Lazima tufikirie katika hili na Watumishi wote itawabidi wavumilie katika kipindi hiki cha mpito na tumekwisha kubaliana kwahiyo baada ya hapo tutaangalia lakini kwa sasa tufanye kazi ya wananchi kwanza” – Robert Gabriel