Leo January 1, 2018 ni sikukuu ya Mwaka Mpya na kila mtu anastahili yake ya kusherekea kuupokea Mwaka Mpaya 2018. Kwa upande wa muigizaji Wastara Juma yeye amesema huwa anaitumia siku ya leo kwa kuangalia picha za aliyekuwa mume wake Sajuki Kilowoko amabaye alifariki January 2, katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Katika ukurasa wake wa Instagram Wastara ameandika “Naweza nikawa nakosea sana lakini sina jinsi ni mapenzi ya dhati ndio yananituma kufanya hivi siwezi kuuzuia moyo Ulipokuja kwenye maisha yangu kuna maisha mapya nimeishi na wewe na umeniacha,”
Wastara aliendelea kupost “Kama kupost picha zako kila mwanzo wa mwaka huwa kunaniletea shida na matatizo katika maisha yangu basi wacha tu yanikute niko tayari kuyapokea lakini hakuna wa kusitisha zoezi hili katika maisha yote mpaka nakufa mwaka mpya nitakuwa na wewe kokote niendapo japo kiroho inanitosha,” – Wastara
KITU PAPI KOCHA KAMFANYIA RAIS JPM, BONYEZA PLAY KUTAZAMA