Nyota wa timu ya Taifa ya Brazil na klabu ya Liverpool, Philippe Coutinho atamaliza hatua yake kuhamia Fc Barcelona katika siku chache zijazo, kulingana na taarifa katika vyombo vya habari vya Hispania. Ripoti ya Leo January 3, 2018 imesema Coutinho amechagua kuvaa jezi namab 7 Barcelona, pia taarifa hiyo ikatokea katika mtandao wa Express.
Upande wa Liverpool wameonesha nia ya kumuongeza mshahara Coutinho na kumpa muda wa utawala ndani ya Anfield.
Ripoti katika gazeti la Barcelona-Based Sport linaamini kuwa uhamisho umekubalika. Kichwa cha habari katika gazeti hilo kimesomeka ‘Coutinho karibu sana’.
Mchezaji huyo wa Liverpool amesema kuwa atakuwa na mkutano Uingereza ili kukamilisha maelezo ya uhamisho katika siku zijazo na amedai hataki kuchezea tena Liverpool.
VIDEO: HAJI MANARA WA SIMBA AMETAJA KILICHOMUUMIZA SANA 2017.
VIDEO: JUMA MAHADHI ALIPOPIGA MAGOTI KUOMBA MSAMAHA YANGA
https://www.youtube.com/watch?v=1oNJmyXQDfo