Leo January 5, 2018 Halmashauri ya Jiji la Arusha imeyafungia maduka manne ya dawa za Binadamu kwa kufanya biashara bila leseni, huku wafanyakazi wake wakiwa hawajakidhi sifa na vigezo vya kitaalamu vinavyohitajika kufanya kazi kwenye maduka hayo jambo ambalo linahatarisha maisha ya watu.
Mganga Mkuu wa Jiji la Arusha Doctor Simon Chacha ambaye pia ni Katibu wa Lishe, Chakula na Dawa amesema wamefanya operesheni kutokana na malalamiko mengi kutoka kwa wagonjwa ambao wamekuwa wakilalamikia kupewa dawa zisizo na sifa ya kutibu maradhi yanayowasumbua na kusababishia wengine kuathirika zaidi na dawa hizo.
MAHAKAMANI: Rugemarila amewataja ‘wezi wa fedha za Escrow’
Muhimbili Hospitali wazungumzia Hali ya Mzee Kingunge