Leo January 8, 2018 Maandamano yamezuka kutokana na kuongezeka kwa bei ya mkate mara mbili ya bei iliyokuwepo na kusababisha kifo na wengine kujeruhiwa nchini Sudan Kusini.
Maandamano yametokea baada ya Serikali ya nchi hiyo kufanya maamuzi ya kuondoa ruzuku ya vyakula na kusababisha gharama ya mkate kuwa kubwa mara mbili zaidi ya bei ya awali.
Katika mji wa Darfur mwanafunzi mmoja katika maandamano aliuawa na wengine sita kujeruhiwa mara baada ya maandamano kugeuka kuwa fujo nako Khartoum, polisi wametumia mabomu ya machozi kuwasambaratisha watu ambao walikuwa wamefunga barabara na kuchoma matairi.
Naibu waziri wa mambo ya ndani alikanusha kuwa maandamano hayajatokea kutokana na ongezeko la bei na kuahidi kuwa atawashughulikia wale wote waliofanya maandamano yenye fujo. Kuongezeka kwa bei ya mkate Sudan ni sehemu ya kufuata matakwa ya IMF ili kukuza uchumi wa nchi hiyo.
VIDEO: JPM ATENGUA UTEUZI AKIMUAPISHA NAIBU WAZIRI WA MADINI