Leo January 9, 2018 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia kwa Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo imetoa taarifa ya unachotakiwa kufanya pale unapopoteza kadi ya usajili wa gari au pikipiki, kwa kupitia kwenye magazeti na kituo cha Polisi.
”Baada ya kutoa taarifa kwenye gazeti, wanapaswa pia kutoa taaarifa polisi ya upotevu wa kadi ya usajili wa gari, hii ni muhimu sana kuepuka usumbufu ambao umekuwa ukijitokeza, kumekuwepo na udanganyifu wa aina mbalimbali-” Richard Kayombo