Leo January 9, 2018 Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imetoa taarifu kwa umma kuwa habari zinazosamba mitandaoni kuhusu sekta ya kibenki nchini kutokuwa salama si sahihi na zinapaswa kupuuzwa.
BOT wamesema kuwa sekta ya kibenki nchini ipo salama na Benki Kuu ipo makini kuhakikisha kuwa sekta ya kibenki na mfumo wa fedha kwa ujumla ni salama na stahimilivu, hivyo Benki Kuu inaendelea kuzisimamia benki zote kwa ukaribu kama inavyotakiwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.