Daraja lenye urefu wa mita 446 nchini Colombia ambalo lilikuwa bado kwenye ujenzi limekatika na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine kujeruhiwa vibaya huku wengine 11 wakiripotiwa kupotea.
Daraja hilo ambalo lilikuwa likitarajiwa kuzinduliwa rasmi mwezi March mwaka huu, lilijengwa kwenye eneo la mlima Chirajara kwa lengo la kuunganisha eneo hilo la Colombia kati na Mji Mkuu wa nchi hiyo uitwao Bogota.
Inaelezwa kuwa baada ya kuvunjika kwa daraja hilo, waliokuwa wanajenga walianguka mita 280 kwenda kwenye korongo jambo lililosababisha vifo hivyo na majeruhi hao.
Kampuni yajifungia kuchapisha GAZETI kwa miezi mitatu na kuomba msamaha kwa JPM na Kagame
Wafanyakazi NAKUMATT walalamikia kukosa mshahara