Leo January 22, 2018 kumetokea ajali ya mabasi mawili madogo ambayo yamegongana uso kwa uso katika Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine watatu kujeruhiwa kwenye ajali hiyo huku chanzo kikitajwa kuwa ni mwendo kasi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mwanza Ahmed Msangi ameongea na waandishi wa Habari katika eneo la tukio namnukuu “basi dogo la kampuni ya Walawi, lilikuwa likitokea Kamanga kwenda Biharamulo liligongana uso kwa uso na basi dogo la kampuni ya Mkombozi, lililokuwalinatokea Sengerema, ajali imesababisha vifo vya watu wawili na majeruhi watatu,”
BREAKING: SAID AMWAGA MACHOZI BAADA YA SCORPION KUHUKUMIWA MIAKA 7