Staa wa muziki Nigeria Peter Okoye kutoka kwenye kundi la Psquare ambaye amekuwa akifanya kazi peke yake kama solo artist tangu kundi hilo liliposambaratika ametangaza ujio wa brand yake ya nguo ambayo itakuja hivi karibuni.
kupitia ukurasa wa instagram wa Peter Psquare ameweka wazi suala hilo baada ya kupost picha akiwa amevaa nguo ambayo itapatikana katika brand ya nguo zake.
“Habari zenu, hii ni kutoka kwenye brand ya nguo zangu,msijali kuhusu maandishi ya jina langu ni kwaajili yangu binafsi . Mnafikiriaje?? Jina la brand ya nguo zangu litatoka hivi karibuni”-Peter Psquare
50 Cent akerwa na maneno ya shabiki kutoka Nigeria