Leo January 30, 2018 Kiongozi mkuu wa Muungano wa upinzani nchini Kenya (NASA) Raila Odinga amejiapisha kuwa ‘rais wa wananchi’, huku serikali ikifungia baadhi ya vituo vya habari vilivyokuwa vinarusha matangazo LIVE.
Odinga alipofika na ‘alikula kiapo’ na kuondoka. Wengi wamekuwa wakimsubiri kwa hamu na hawakutegemea kwamba atachukua muda mfupi hivyo katika uwanja wa Uhuru Park.
Odinga alifika katika uwanja wa Uhuru Park akiwa na viongozi kadha wakuu wa NASA na kujiapisha akishika Biblia. Amewaambia kuwa mgombea mwenza Kalonzo Musyoka wa chama cha Wiper ataapishwa baadaye.
Viongozi wengine wenza wa Nasa Moses Wetangula na Musalia Mudavadi pia hawakufika katika wuanja huo. Odinga amesema leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya.“Hatua ya leo ni kuelekea kutoa udikteta na kuleta demokrasia Kenya, Maelekezo mengine mtayapata baadae”
Raila Odinga alimwambia mwandishi wa kituo cha habari cha KTN kwamba shughuli hio ‘ si mapinduzi ya serikali’
BREAKING NEWS: NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA