Ilikuwa ni mshikemshike mkubwa pindi Hyatt Regency hoteli ambayo zamani ilijulikana kama Kilimanjaro Kempinsky ya jijini Dar es Salaam kutangaza ofa ya chumba cha milioni 22 na laki 4 kwa ajili ya Siku ya Wapendanao yaani Valentines Day.
Inaelezwa kuwa chumba hiki ni kile wanacholala marais pindi wakija nchini na kwa siku za kawaida bei yake huwa ni Dola za Marekani 5000 sawa na Tsh Milioni 11 za Kitanzania.
Uongozi wa hoteli hiyo umetangaza kuwa simu zimemiminika tangu kutangazwa kwa ofa hiyo jana.
Kutokana na hilo Ayo TV na millardayo.com zimetafuta taarifa kuhusu hoteli 10 Duniani ambazo ni za gharama za juu zaidi.
10. Park Hyatt – Paris Ufaransa
Gharama ya hoteli hii kwa kulala usiku mmoja ni Dola za Marekani 15000 ambayo ni sawa na Tsh Milioni 36.
9. Four Seasons Hotel George V.
Hii ni hoteli iliyopo pia Paris nchini Ufaransa. Gharama ya chumba kwenye hoteli hii ni Dola 1, 500 kwa usiku mmoja sawa na Tsh. za Kitanzania Milioni 37.2
Hii ndiyo hoteli ya kifahari zaidi Paris lakini inashika namba 9 kwenye orodha ya hoteli za kifahari na za gharama zaidi duniani.
8. Le Richemond – Geneva, Uswisi.
Kulala usiku mmoja kwenye hoteli hii inakulazimu uwe na kiasi cha Dola 17,000 ambayo ni sawa na Tsh za Kitanzania Milioni 40.8.
Hii pia ni moja ya hoteli mbili za kifahari zaidi zinazopatikana nchini Uswisi na hii ndio ya gharama ya chini.
7. Burg Al Arab – Dubai
Bei yake kwa usiku mmoja kwenye hoteli hii ni Dola 17500 ambayo ni sawa na Tsh Milioni 42 za Tanzania.
Inaelezwa kuwa sio watalii tu wanaipenda hoteli hii bali mamilionea na watu maarufu Duniani kote husafiri kutoka kwenye makazi yao ili kufikia kwenye hoteli hiyo.
Uzuri wa hoteli hii umefanya eneo iliyopo kwa maarufu sana Dubai.
6. Ritz- Carlton – Moscow, Urusi
Hoteli hii ni ya gharama Dola 17,500 ambayo ni sawa na Tsh Milioni 42 za Tanzania kwa usiku mmoja.
Hoteli hii ni maarufu Duniani kwani ni ya siku nyingi na ubora wake haujashuka. Inaelezwa kuwa imekuwa kwenye orodha hii ya hoteli za kifahari Duniani kwa miaka mingi sana.
5. Atlantis Resort Hotel – Bahamas, Dubai
Gharama yake kwa usiku mmoja ni Dola 24,000 ambayo kwa pesa ya Tanzania ni sawa na Tsh Milioni 57.6.
4. President Wilson Hotel – Geneva, Uswisi
Kulala kwenye hoteli hii ya kifahari nchini humu kwa usiku mmoja itakugharimu Dola 31,500 ambayo ni Tsh za Tanzania Milioni 75.6.
3. Four Seasons Hotel – Manhattan, New York
Hoteli iko nchini Marekani na inagharimu Dola 32,500 ambayo ni takriban Tsh za Kitanzania Milioni 78 pia kwa usiku mmoja tu.
Inaelezwa kuwa watu wanaoweza kukaa kwenye hoteli hii ni wale ambao wanauhakika wakutokuja kufilisika maisha yao yote.
2. Palms Cassino Resort Hotel – Las Vegas Marekani
Hoteli hii kulala kwa usiku mmoja tu inakubidi ulipe Dola 38000 ambayo ni sawa na Tsh Milioni 91.2 za Tanzania. Ni hoteli maarufu sana kwa matajiri ambao ni wapenzi wa michezo ya kamari.
Inaelezwa kuwa wakati mwingine mteja wa kudumu wa hoteli hii anaweza kupewa chumba cha kulala bure ilimradi tu ijulikane kuwa mteja huyu atatumia mamilioni ya pesa kwenye casino yao.
1. The Grand Resort Lagonissi – Anthens Ugiriki
Hii ndiyo hoteli ya gharama kubwa kuliko hoteli zote duniani. Kwenye hoteli hii usiku mmoja wa kulala ni Dola 47500 ambazo ni sawa na pesa za Tanzania Tsh Milioni 114.
MSEMAJI WA SERIKALI ANAZUNGUMZIA “HALI YA UCHUMI WA TANZANIA”