Habari kutoka Kenya ni kuhusu sakata la ‘kujiapisha’ kwa Kiongozi wa Muungano Upinzani NASA Raila Odinga na wote waliohusika kwa namna moja au nyingine, zinaendelea na leo Mahakama ya Juu nchini Kenya imetoa amri mpya kwa Jeshi la Polisi.
Mahakama imeamuru Jeshi hilo la Polisi kuacha kuwakamata au kuwabugudhi kwa namna yoyote ile Manager Mkuu wa Kampuni ya Nation Media Group (NMG) Linus Kaikai na waandishi wawili Larry Madowo na Ken Mijungu.
Watatu hawa wamekuwa wakiishi kwa mashaka na hofu ya kukamatwa na Polisi kutokana na kuhusishwa na tukio la ‘kujiapisha’ Raila Odinga, ambapo serikali iliifunga mitambo vya televisheni za KTN, Citizen TV na NTV na baadaye Mahakama kuamuru mitambo hiyo ifunguliwe.
Wema Sepetu baada ya kutoka Mahakamani
Alichozungumza Diamond Platnumz baada ya Kesi yake na Hamisa