Leo February 12, 2018, kutoka millardayo.com tumepata hii kali kumhusu mwanamke mmoja ambaye ana umri wa zaidi ya miaka 80 nchini Uingereza ameripotiwa kulala bafuni kwake kwa siku tatu mfululizo baada ya kujifungia kwa bahati mbaya alipoingia.
Inaelezwa kuwa bibi alishindwa kutoka wala kupatiwa msaada kwasababu anaishi peke yake na hana mtu wa karibu wa kumtunza, hivyo hali hiyo imemlazimu bibi huyu kukaa chooni humo kwa siku hizo zote.
Hatahivyo jirani mmoja ambaye ndiye aliyetoa taarifa kwa polisi amedai kuwa aliona mapazia ya nyumba ya bibi huyo hayajafungwa kwa siku tatu mfulizo ikiwa ni pamoja na viashiria vingine ambavyo vilimpa wasiwasi na kuamua kuwaita maaskari.
Maaskari walipofika eneo la tukio ilibidi wavunje mlango na kumtoa bibi huyo. Hata hivyo wito umetolewa kwa watu kuwajali wazazi au ndugu zao ambao wameshakuwa wazee kwa kuishi nao, kufanya mawasiliano nao pamoja na kuwatembelea mara kwa mara.
Tukiamua kufata sheria kama nchi nyingine ”HAULIPWI KITU”- Naibu Waziri
RC Mongella na Kamati ya Ulinzi na Usalama walivyofanya kazi ya kupasua na kubeba Mawe