Stori nayokusogezea leo February 25, 2018 ni kumhusu Msichana mwenye umri wa miaka 25, Anastazia Elias, mkazi wa Kata ya Kipindu wilayani Nkasi mkoani Rukwa, amenusurika kifo baada ya kuokolewa na polisi akituhumiwa kumuua mtoto wake baada ya kujifungua.
Wananchi wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mawe walianza kumshambulia mwanamke huyo wakimtuhumu kumuua mwanawe wa kiume baada ya kujifungua ambapo alimviringisha na vipande vya khanga na kumuweka kwenye kikapu alichokificha chini ya uvungu wa kitanda chake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea juzi saa nane mchana katika Kijiji cha Kipundu kilichopo mjini Namanyere.
Kamanda Kyando amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Polisi wilaya Nkasi na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa tukio kukamilika. Wakizungumza baadhi ya wanawake wamedai mtoto huyo alizikwa juzi usiku katika kaburi lililochimbwa ndani ya nyumba ambayo mama yake mzazi anaishi na bibi yake.
Akisimulia tukio hilo, Diwani wa Kata ya Kipundu, John Kapandila alisema mchana wa siku ya tukio, watoto wadogo walimuona mwanamke huyo akiwa amebeba kitu kwenye mfuko wa plastiki na kwenda chooni alipotoka hakurudi nao. “Watoto hao walikimbia na kuwataarifu wazazi wao kuwa Mama Baraka amejifungua mtoto, lakini amemtupa chooni.
RPC Kinondoni amezungumza kuhusu Majeruhi wa Risasi waliopo OYSTERBAY Polisi