Stori nayokusogezea Leo March 1, 2018 ni kuhusu Rufaa ya kupinga hukumu ya kifungo cha miezi mitano jela aliyohukumiwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga imewasilisha Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.
Wakili wa Sugu na Masonga, Faraji Mangula amesema tayari maombi ya rufaa yao yamepokelewa leo na kupewa kumbukumbu namba 29/2018.
“Tayari rufaa yetu imeshapokewa Mahakama Kuu Mbeya na tunachosubiri ni kupangiwa tarehe ya kuanza kusikiliza tu, ila tunachoshukuru watu wa Mahakama hii wapo vizuri kushughulikia suala hili,” -Mangula.
Licha ya kukata rufaa pia Mawakili hao wanakusudia kuomba dhamana kwa wateja wao ili waweze kuwa nje katika kipindi ambacho wanakuwa wanasikiliza rufaa yao.
Sugu na Masonga walihukumiwa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.
SHUGHULI ZA MAHAKAMA YA KISUTU ZA SIMAMA BAADA YA MOTO KUZUKA