Habari za Mastaa

‘Kati ya nyimbo zote, nyimbo mpya peke yake ni yangu’ -Ney wa Mitego

on

Leo March 1, 2018 stori zinazohusiana na TCRA kupiga marufuku baadhi ya nyimbo kuchezwa katika TV na Redio zinaendelea kushika headlines ambapo  Staa wa Muziki wa Bongo Fleva Emmanuel Elibariki, maarufu kama Ney wa Mitego amesema yeye ndio chanzo cha kufungiwa kwa nyimbo nchini.

Nyimbo zaidi ya kumi zilitangazwa na Mamlaka ya Mawasiliano kupigwa marufuku kuchezwa katika redio na TV Tanzania.

“Wakati mwingine naona kuwa sababu ya kufungiwa kwa miziki hii ni mimi na wengine wanawekwa kama chambo kwa kuwa kati ya nyimbo zote hizo, nyimbo mpya peke yake ni yangu tu ambayo imetoka wiki mbili zilizopita na video ina wiki moja tu” -Ney wa Mitego.

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa mwanamuziki huyo kupata misukosuko katika muziki wake. March 2017, Ney wa Mitego alikamatwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuimba wimbo unaokashifu serikali.

NYIMBO 13 ZA BONGOFLEVA, TCRA IMEAGIZA ZISIPIGWE REDIONI WALA TV

Soma na hizi

Tupia Comments