Kamishna wa Operation na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, CP Nsato Marijani leo March 9, 2018 amezungumza na vyombo vya habari ametoa onyo kwa kikundi kinachohamasisha maandamano kupitia mtandao wa Telegram na kusema jeshi hilo litafanya kila liwezekanalo kisheria kukizuia.
CP Marijani ameeleza kuwa kikundi hicho kimepanga maandamano ya nchi nzima kinyume cha sheria na kutaka kwenda Ikulu, na kwamba lolote linalofanyika nchini lazima lifanyike kwa mujibu wa sheria.
“Ukifanya maandamano kwa nia ya kuiondoa serikali ni uhaini, na uhaini ni kosa kubwa, Jeshi la Polisi linaomba wazazi na walezi wawakanye watoto wao wanaotaka kushiriki kwenye maandamano hayo kuacha kwani hilo ni kosa la uhaini.” – CP Marijani
“Ngoja waandamane wataniona” – JPM