Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2018 imeendelea tena leo kwa mchezo wa Yanga dhidi ya Kagera Sugar kuchezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam, huo ukiwa ni mchezo muhimu kwa Yanga kuweza kuwafikia wapinzani wao Simba ambao mchezo wao wa mwisho wa VPL dhidi ya Stand walipata sare ya 3-3 na kupunguza gape la point.
Yanga waliyokuwa na kiporo cha mchezo mmoja wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Kagera Sugar na kutimiza jumla ya michezo 20 sawa na Simba, huku wakiachwa point tatu na Simba baada ya ushindi wa leo kuwafanya wafikishe jumla ya point 43.
Magoli ya Yanga yalifungwa na staa wao Ibrahim Ajib dakika ya 53 kwa mkwaju wa penati, Yusuph Mhilu aliyetumia vyema kazi za Ajib na Chirwa wakati goli la mwisho Kagera Sugar wakijifunga wenyewe dakika ya 88 kupitia kwa Juma Shemvuni.
UTANI MWINGINE HUU: Mkaliwenu baada ya sare ya 2-2 ya Simba SC vs Al Masry