Leo March 14,2018 story inayo-trend kwenye mitandao ya kijamii ni kuhusu staa wa muziki kutokea Marekani Zayn Malik na mwanamitindo Gig Hadid kuachana ikiwa wamefanikiwa kukaa kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa miaka miwili ambapo mahusiano yao yalianza mwaka 2016.
Kupitia twitter account ya Gig Hadid amethibitisha kuachana kwake na Zayn Malik ingawa mashabiki hawajafurahishwa kuachana kwa wapenzi hawa maana ni couple ambayo ilikuwa ikipendwa na watu wengi.
“Taarifa za kuachana huwa sio taarifa binafsi kwasababu huwa hakuna namna nzuri ya kuelezea wahusika wenyewe wanapitia nini katika kipindi cha miaka michache waliokuwa pamoja, sio tu kwenye mahusiano bali hata katika maisha ya kawaida”
“Nina shukuru kwa upendo, muda na mafunzo ya maisha ambayo mimi na Z tumeyapata. Sihitaji kingine zaidi ya mema kwa Z na nitaendelea kumsaidia kama rafiki ambaye nina mheshimu na kumpenda.”
“Kwa siku zijazo, chochote kilichopangwa kutokea kitatokea”
Dogo Janja kwa wanaokosoa idea ya kujitumia kama video vixen