Leo March 14, 2018 kupitia Clouds FM, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo Juliana Shonza na Katibu wa BASATA Mwingereza pamoja na baadhi ya wasanii akiwemo msanii wa hip hop Wakazi na Vanessa Mdee ambapo walikuwa wakizungumzia ishu ya ufungiaji wa nyimbo za wasanii na mengineyo..
Sasa Millardayo.com inakusogeza baadhi ya mambo kumi makubwa yaliyojadiliwa siku ya leo kupitia kipindi cha XXL ya Clouds FM..
“Kimsingi Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na michezo ina kazi nyingi pamoja chini yake kuna vyombo vingi vya kusimamia kazi hizo kama BASATA na BAKITA. Tangu nimeapishwa kuwa Naibu Waziri niliapa kulinda maadili katika Wizara ambayo ninaifanyia kazi” -Naibu Waziri Shonza
“Kumekuwepo sana upotofu wa maadili mpaka Rais akaamua kuweka msisitizo. ndio maana nimeweka sana msisitizo kwenye hili japokuwa kuna changamoto nyingi zinazoikumbuka sanaa kiujumla” -Naibu Waziri Shonza
“Inapotoka taarifa rasmi ya kufungiwa kwa wimbo wa msanii, inajumuisha Audio na Video ambayo imekiuka maadili husika ya kanuni za sanaa za nchi, kuna wasanii ambao wanafanya vizuri sana kama Monalisa na Mzee Majuto hawa wanafanya vizuri lakini Hawavai vibaya tunataka wasanii waige mfano wao.” Naibu Waziri Shonza
“Kwa mfano Alikiba ni msanii mkubwa wa kimataifa, anaiwakilisha nchi vyema, lakini haimbi nyimbo lugha chafu wala video ambazo hazina maadili. Sisi kama wizara tunataka sanaa iende pamoja na ukuaji wa maadili ya nchi – tutoe burudani lakini tulinde utamaduni wetu.” – Naibu Waziri Shonza
“Wizara ya Sanaa inaona makosa tu na kutoa adhabu lakini wasanii hawajawezeshwa, mnatuhukumu kwa tafsiri za maneno kutokana na mnavyoelewa nyinyi japokuwa sisi huwa hatumaanishi neno mlivyoelewa nyinyi. Hii si sawa. Kuna changamoto nyingi za msingi na za maana ambazo mlitakiwa kama wizara kuanza kuzishughulikia.”– Msanii Wakazi
‘Ule wimbo wa Bongo Bahati mbaya umekiuka misingi ya nchi, unaondoa dhana ya kujivunia Utanzania. Ndio maana kuna watu wanasema bora kuzaliwa mbwa ulaya kuliko kuzaliwa Tanzania. Tumeufungia kwa kufuata kanuni na sheria.” Katibu BASATA
“Kwenye ile listi ya nyimbo zilizofungiwa kulikuwa na makosa ya kimaandishi na kisarufi. Hivi ni vitu vidogo lakini vinaonyesha wazi kwamba hakuna umakini katika ufuatiliaji wa kina wa kazi. Haiwezekani Baraza halijui jina halisi la msanii ambaye linamfungia kazi zake.”
Pia nawaomba angalieni adhabu mnazotoa kwa wasanii, Roma amefungiwa miezi 6, yeye ni baba, ana mke mjamzito, miezi 6 hii anatoa wapi hela ya kuendesha familia yake. Tunaomba mliangalie hili. Toeni adhabu nyingine ila tuachwe tufanye kazi. – Vanessa Mdee
“Sisi tunafanya kazi na wadau wa Muziki kuna watu wanatusaidia kufanya Hizi kazi mkiwemo nyingi watangazaji.”
“Mimi niliapa kwa katiba kwahiyo naangalia Sheria na kanuni zinasemaje, hizo ndio zinazoniongoza.” Naibu Waziri Shonza
Mbasha “Ninauwezo wa kwenda Mahakamani, sioni sababu ya Flora kuninyima mtoto”
Tunda na Casto Dickson wamezungumza “Tukiwa wapenzi kuna ubaya gani?”