Bado stori za kocha wa Man United Jose Mourinho kutokuwa katika maelewano mazuri na kiungo wake raia wa Ufaransa Paul Pogba zinazidi kuchukua headlines, jana March 20 kocha wa Ufaransa alisema kuwa Paul Pogba amekiri kuwa hana furaha ndani ya club ya Man United kufuatia kuwekwa benchi na stori mbalimbali zinazoendelea nje ya uwanja.
Leo mtandao wa dailymail.co.uk umeripoti kuwa Jose Mourinho pia hajafurahishwa na kitendo cha Paul Pogba kumpongeza kwa kumvuta mkono wakati Mourinho anafanya interview na BBC baada ya ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Liverpool, pamoja na kuwa Mourinho alionesha kutabasamu mbele camera za waandishi lakini hakupenda kitendo hicho cha Pogba.
Pogba hajapata nafasi ya kuanza chini ya Jose Mourinho toka March 10 2018, inaripotiwa kuwa baada ya interview Mourinho alimueleza na kumuonya Pogba kuhusiana na kitendo hicho kuwa hajafurahishwa nacho, Pogba alijiunga na Man United 2016 akitokea Juventus ya Italia kwa pound milioni 89 lakini anapitia wakati mgumu kwa sasa ndani ya Man United kiasi cha kuripotiwa kuwa hana furaha.
Hivi ndio Simba walivyotoka sare ya 2-2 dhidi ya Al Masry