Jaji Mkuu wa Mahakama ya Juu Hispania amesikiliza kesi ya viongozi 13 wakubwa wa Jimbo la Catalonia nchini Hispania, wakikabiliwa na mashtaka ya uasi juu ya majukumu yao katika kura ya maoni na tamko la uhuru mwaka 2017.
Inaelezwa kuwa ikiwa viongozi hao watakutwa na hatia, wanaweza kuhukumiwa hadi miaka 25 jela. Viongozi hao ni pamoja na Rais Mstaafu wa Jimbo hilo Carles Puigdemont na Jordi Turul ambaye kesho anatarajiwa kupigiwa kura ya kuchukua nafasi hiyo.
Jaji huyo Pablo Llarena ameeleza kuwa viongozi hao kwa kushirikiana na vikundi vya asasi za kijamii kwa miaka sita iliyopita wamefanya njama kusuka mpango wa kutangaza Uhuru wa Catalonia, jambo lililo kinyume na utaratibu wa kisheria nchini Hispania.
Mahakama imetoa tamko hilo leo March 23, 2018 na kusema kwa ujumla imetoa hukumu hiyo kwa makosa ya kuasi, rushwa na kutotii kwa viongozi hao.
“Hali ni mbaya, watu 77 wanafariki kwa siku” –Waziri Ummy Mwalimu