Mbunge wa Mtwara mjini Maftaha Nachuma alisimama Bungeni Dodoma leo April 5, 2018 na kulieleza Bunge kuhusu Jeshi la Polisi kikosi kazi cha Maliasili kumpiga risasi ya kisogoni iliyompelekea kufariki mtu mmoja aliyekuwa akijitafutia kitoweo katika ufukwe wa bahari.
Maftaha amesema..>>>“Tarehe 25 mwezi wa tatu pale Mtwara mjini kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Abilah Abdureheman alikuwa katika ufukwe wa bahari akijitafutia kitoweo, wakati anajitafutia kitoweo hicho ghafla walitokea Jeshi la Polisi ambao ni kikosi kazi cha Wizara ya maliasili wakamuita kijana akakimbia Askari wakaamua kumpiga risasi kisogoni”
Agizo la Waziri Nchemba kwa Jeshi la Polisi “msiwaachie”