Leo April 16, 2018 Serikali ya Israel imesema ina mpango wa kuwaachilia huru wahamiaji wa Kiafrika 200 ambao wamefungwa katika gereza la Jangwani nchini humo.
Israel imekuwa ikijaribu kufikia makubaliano na Uganda kuwachukua wahamiaji hao walioingia nchini humo kwa miguu kupitia mpaka wa Misri.
Wafungwa hao wanaotarajiwa kuachiliwa huru, walipelekwa katika gereza la Jangwani katika miezi ya hivi karibuni kusubiri safari ya kupelekwa nchini Uganda.
Serikali ya Israel imesema wahamiaji 37,000 waliopo nchini humo wanatafuta kazi na kwamba, ina kila haki ya kulinda mipaka yake.
Alichozungumza Fatma Karume baada ya kushinda urais TLS