Leo April 21, 2018 Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un amefanya uamuzi kusitisha majaribio ya makombora na kufunga maeneo yote yaliyokuwa yakitengeneza silaha za Nuklia.
Shirika la habari la Korea Kaskazini lilitangaza kuwa “Kuanzi leo, Aprili 21, Korea Kaskazini inaachana na majaribio ya nuklia pamoja na uzinduzi wa makombora ya kisasa,”.
Kim amesema kuwa majaribio hayo sasa siyo ya muhimu sababu uwezo wa masuala ya Nuklia wa Korea Kaskazini “umeshathibitishwa”.
Tangazo hilo la kushtukiza limekuja wakati Korea Kaskazini ikijiandaa kufanya mazungumzo ya kihistoria na nchi ya Marekani na Korea Kusini.
Rais wa Marekani baada ya tangazo hilo ameandika katika ukurasa wake wa Twitter “Hii ni hatua nzuru na habari njema kwa Korea Kaskazini na Dunia kwa ujumla!”.