Mtoto wa Rais wa kwanza wa taifa la Guinea Ahmed Sékou Touré anayefahamika kwa jina la Mohamed Touré na mkewe Denise Cros-Touré wanatuhumiwa kwa kujihusisha na utumwa.
Inaelezwa kuwa wawili hao ambao wote wana umri wa miaka 57 wanashutumiwa kukaa na binti wa miaka 16 kama mtumwa nyumbani kwao Texas Marekani.
Jina la mtoto mpya wa kifalme Uingereza latajwa
Wanadaiwa kumchukua kutoka Guinea kwenda Texas akiwa na miaka mitano na wamekuwa wakimtumikisha binti huyo kwa kazi za nyumbani, huku akiwalea watoto wao na kumfanyia unyanyasaji mwingine.
Kipindi chote hicho binti huyo hakupelekwa shuleni na walimnyang’anya nyaraka zake za kusafiria na kumlazimisha kuendelea kuishi Marekani hata kipindi ambacho visa yake ilikuwa imekwisha muda wake.
Tukio la kuuawa watoto 140 wakati mmoja kama sadaka lagundulika
Mtoto huyo anadaiwa kutoroka kwa msaada wa majirani na kama wawili hao watakutwa na hatia basi watafungwa kifungo cha hadi miaka 20 jela.
Mohamed Touré kwasasa ni Katibu Mkuu wa chama cha Democratic Party of Guinea (DPG) ambacho kiliasisiwa na baba yake.
Lema amezungumza “Nimejiandaa kisaikolojia leo kwenda rumande”