Jana Ijumaa ya April 27 2018 kiungo wa FC Barcelona Andres Iniesta alitangaza rasmi mbele ya waandishi wa habari kuwa anaondoka timu hiyo, moja kati ya watu ambao wamechukua headlines ni Lionel Messi kutoonekana wakati Andres Iniesta anaaga, hivyo imezua maswali mengi kutokana na wawili hao wamecheza kwa pamoja muda mrefu.
Leo imegundulika sababu ya Lionel Messi kutokuwepo wakati Iniesta anaaga ni kutokana na yeye na familia yaku kuwa busy na kushughulikia passport zao mpya, hivyo alikuwa hana budi kuikosa siku ya Iniesta ambaye ameaga kuwa msimu huu ndio mwisho kuichezea FC Barcelona na ataondoka.
Lionel Messi ambaye ni mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or mara tano kwa pamoja yeye na Andres Iniesta wamecheza FC Barcelona toka 2004 Messi akiwa na umri wa miaka 17 na Iniesta akiwa na umri wa miaka 20, Iniesta anaondoka FC Barcelona na amesema kuwa anaenda kucheza nje ya bara la Ulaya kutokana na kuwa hahitaji kucheza dhidi ya FC Barcelona.
VIDEO: Mapokezi ya Yanga Airport DSM na alichokisema kocha wao