Muigizaji wa filamu za ngono Stormy Daniels amefungua mashtaka dhidi ya Rais wa Marekani Donald Trump juu ya kile anachodai kuwa Trump ame-tweet ujumbe ambao ‘umemchafulia’ jina lake.
Muigizaji huyu ambaye jina halisi ni Stephanie Clifford ameeleza kuwa amepokea vitisho akiwa kwenye eneo la maegesho ya gari ili mjini Las Vegas na kutakiwa kuacha kuendelea na madai yake ya kuwa na uhusiano na Trump.
Inaelezwa kuwa Trump ali-tweet mchoro wa mwanaume huyo anayedaiwa kumtishia Stormy na kuandika ujumbe unaosema “hii ni kazi ya utapeli kabisa” na baadaye kujibiwa na wakili wa Stormy kwenye Twitter akisema Trump “anafahamu vyema kabisa yaliyotokea”.
Kesi iliyowasilishwa katika mahakama ya dola mjini New York inasema “Trump alitumia fursa ya mamilioni ya watu wanaomfuatilia katika mtandao huo wa Twitter kutoa taarifa ya uongo yenye lengo la kumshushia hadhi na kumshambulia Bi Clifford.“
Waziri Mwakyembe baada ya kuwapokea Serengeti Boys na Kombe