Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe alisimama Bungeni baadhi ya changamoto zilizopo katika sekta ya elimu nchini wakati akiwasilisha taarifa ya kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na maendeleo ya jamii ambayo yeye alikuwa mjumbe.
“Elimu yetu bado inakumbana na changamoto nyingi, matokeo ya mwaka 2014 ya Bank ya dunia yanaonesha kuwa Asilimia 20 ya walimu vijijini na asilimia 36 ya walimu mjini hawakuwepo shuleni wakati asilimia 53 ya walimu walikuwepo shuleni lakini hawaingii madarasani”
“Kwa mujibu wa ripoti ya Twaweza imeeleza kwamba ni mwanafunzi mmoja kati ya kumi (13%) wa darasa la tatu aliweza kusoma stori ya kiingereza wakati kwa mwanafunzi wa darasa la 7 ni wanafunzi 5 kati ya 10 ndio waliweza kusoma stori hiyo”
“Kuna siku watu wataujua ukweli na watashangaa” –Prof Tibaijuka