Wanasoka wenye jinsia ya kike nchini Iran hivi sasa wanatakiwa kabla ya kushiriki kwenye mechi za mchezo huo kufanyiwa vipimo vya kugundua jinsia – hatua hii imekuja baada ya wanasoka kadhaa nchini humo – wakiwemo wanne kutoka katika timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Iran kugundulika kuwa walikuwa ni wanaume.
Wachunguzi wa kitabibu watakuwa wanavamia bila taarifa katika mazoezi ya timu za wanawake zinazoshiriki katika ligi kuu ya soka la wanawake nchini humo ili kujaribu kuwagundua wanawake wanaojifanya wanawake na kucheza pamoja.
Pia imewekwa sheria mpya ya kuvilazimisha vilabu kufanya vipimo vya afya ya jinsia kwa wachezaji wapya kabla ya kuwasajili kimikataba, hii ni kwa mujibu wa Ahmad Hashemian, mkuu wa shirikisho la soka la Irani kwenye upande wa kamati ya afya.