Moja kati ya stori zilizochukua headlines katika magazeti ya Tanzania ni pamoja na stori ya utafiti iliyokuwa inaeleza kuwa ulaji wa vitu vigumu wakati wa kufturu kunaweza kusababisha saratani ya utumbo , kutokana na mtu anayefunga anashinda kutwa nzima bila kula kitu.
AyoTV imeongea na Dr Kihesa kutoka taasisi ya saratani ya Ocean Road na kutoa ufafanunzi kuhusiana na utafiti huo, Dr Kihesa ameeleza kuwa saratani sio ugonjwa unaojitokeza kwa ghafla unaweza kujitokeza hata baada ya miaka 1o au 15 baadae licha ya kutumia kitu kinachoweza kuleta kansa.
Hata hivyo Dr Kihesa pia ameeleza na kushauri utumiaji wa nyama nyekundu unaweza kusababisha saratani pia lakini vyakula vya kutumia wakati wa kufturu ili kuepuka ugonjwa wa kansa ni bora kuanza na kimiminika chenye uvuguvugu ili kupasha tumbo moto na kuepuka upataji wa ugonjwa wa kansa ya utumbo kwa miaka ya baadae.
VIDEO: January Makamba amebuni njia mbadala kupitia Viongozi wa Dini