Story iliyochukua headlines siku kadhaa zilizopita ni kuhusu harusi ya kifahari “Royal Wedding” iliyofungwa na Prince Harry pamoja na mke wake Meghan Markle, hivyo wengi kutaka kufahamu tamati ya sehemu ya kupumzikia (Honeymoon) kwa wawili hao itakuwaje.
Kupitia mtandao wa TMZ wanandoa hao wameamua kujipumzisha kwa mara ya kwanza kama mume na mke katika hoteli ya kifahari ya Alberta’s Fairmont Jasper Parl Lodge iliyopo Canada ambapo bei ya chumba kimoja ni dola za Kimarekani 6000 zaidi ya shilingi millioni 13 za Kitanzania kwa usiku mmoja.
Maamuzi hayo yanakuja baada ya wawili hao kudaiwa kuweka bara la Afrikakatika katika list ya nchi wanazoweza kwenda kwa ajili ya HoneyMoon ikitajwa nchi ya Namibia.
Inaripotiwa kuwa chumba wanachopumzikia wawili hao kwa ajili ya honey moon katika hoteli ya Alberta’s Fairmont Jasper Parl Lodge kiliwahi kutumika na King George pamoja na Queen Elizabeth 1939 pia Queen Elizabeth II na Prince Philip 2003.
Mtu mmoja Tanzania anakunywa Lita 47 za Maziwa