Baada ya May 24 kutoka kwa taarifa kutoka kituo cha TV cha CNN kudai kuwa muigizaji mkongwe wa movie Hollywood Morgan Freeman kudaiwa kukumbwa na kashfa ya shambulio la ngono kwa wanawake mbalimbali, wanasheria wa muigizaji huyo walipinga taarifa hizo na kueleza kuwa za uongo.
Leo CNN wametoa taarifa kuhusiana na mashtaka yalitolewa na upande wa mwanasheria wa Morgan Freeman na kueleza kuwa kama CNN wanasimamia msimamo wa taarifa walizozitoa kuwa ni ukweli mtupu na watazisimamia kwa ushahidi, CNN pia wameeleza kuwa hoja za upande wa mwanasheria wa Morgan hazina nguvu na zinalenga kuficha ukweli.
Tuhuma hizo za Morgan kutenda kosa la shambulia la ngono inasemekana alifanya mwaka 2015 akiwa katika utengenezaji wa filamu ya “Going In Style” na mmoja kati ya wanawake waliokuwa wakifanya nae kazi hiyo, anadaiwa kutenda kosa la unyanyasaji wa kingono.
Wema Sepetu ameenda kufanyiwa upasuaji India, mahakama imetoa maagizo