Mwanadada Sophie Brussax anayedaiwa kuwa na mtoto mmoja na Rapper Drake kutokea Canada apewa ofa ya Milioni 200 na Website ya Camsoda kufanya mahojiano live kwa saa moja kuongelea kuhusiana na tetesi zinazomkabili kuzaa na rapper huyo.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ unadai kuwa website hiyo ya Camsoda imempa mwanadada huyo ofa mbili ikiwemo kukubali dili hilo la dola 100,000 zaidi ya Milioni 200 za Kitanzania au kucheza filamu ya ngono ili kumkomoa Drake kwa kitendo alichofanya.
Mwanadada huyo Sophie Brussax hajatoa jibu bado kuhusiana na dili hizo mbili alizopewa siku ya Jumatano May 30,2018 ambapo alipelekewa barua na Camsoda ,huku tetesi zingine zikidai kuwa Drake hajakimbia majukumu wala kumtelekeza mtoto wake “Adion” bali anatimiza majukumu yote kama baba.
MPOTO AMKALISHA MAKAMBA/ SHOLO MWAMBA AONDOKA NA KIJIJI