Walinzi 10 wa Kampuni ya KK wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 2 ikiwemo wizi wa mapipa 26 ya Makinikia ya madini ya Tuntulum yenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.7.
Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri kuwa waahtakiwa wapo 11 na wana mashtaka washtakiwa mawili.
Akiwasomea hati ya mashtaka wakili Mwita amedai kuwa April 21,2018 katika jiji la Dar es salaam washtakiwa kwa pamoja wakïwa na wenzao ambao hawapo mahakamani walikula njama ya kutenda kosa la wizi.
Pia Mwita amedai kuwa siku hiyo ya April 21,2018 maeneo ya Tabata Relini wilaya ya Ilala washtakiwa hao bila ya kuwa na uhalali waliiba mapipa 26 ya makinikia ya madini ya Tuntulum yenye thamani ya Sh.Bilioni 1,705,296,434.4 mali ya kampuni ya Ballore Logistics.