Staa wa muziki kutokea Nigeria Falz ambaye anatamba na ngoma yake ya “This Is Nigeria” amepewa siku saba kufuta video hiyo kutoka kwenye mtandao wa You Tube na kikundi cha kutetea haki za Waislamu cha Nigeria(MURIC).
Kikundi hicho cha MURIC kinadai kuwa wimbo huo umevunja sheria za Kiislamu kutokana na staa huyo kuwatumia wasichana waliovaa hijab kwenye video yake ya “This Is Nigeria” na hivyo Falz kujitetea kuwa aliwatumia wasichana hao kufikisha ujumbe kuhusu wasichana wanaoshikiliwa na Boko Haram.
Mkurungezi wa MURIC ameonekana kutovutiwa na jibu alilolitoa mwanamzuiki huyo na kumtaka afute video hiyo na kumtaka awaombe Wanigeria msamaha na kudai kuwa video hiyo imetia uchochezi wa kidini na ikishindikana kufanya hivyo basi atachukuliwa hatua za kisheria.
Waziri wa Uganda azungumzia maamuzi ya Uganda juu ya Bandari ya DSM