Leo June 8, 2018 nakusogezea Utafiti uliochapishwa katika jarida la “Mazoezi ya matibabu” huko Uingereza limefafanua uhusiano kati ya maisha marefu na kasi ya kutembea.
Wanasayansi wa Uingereza na Australia wameelezea kwamba watu wanaotembea haraka si rahisi kupatwa na ugonjwa wa moyo.
Imeonekana kwamba wale walio na umri wa miaka 60 au chini ya hapo ambao wanatembea haraka wamepunguza hatari ya kufariki kutokana na magonjwa ya moyo kwa asilimia 53.
Watafiti wanasema kwamba kasi ya Kilomita 5 hadi 7 kwa saa ni ya kutosha.
Madaktari wanaamini lengo kamili ni kuharakisha mapigo ya moyo na kutokwa na jasho wakati wa kutembea.
Waendesha magari nchini Uingereza ambao hutumia angalau nusu saa kufanya mazoezi na kula vyakula vya afya basi hurefusha maisha kwa miaka kumi.